Friday, January 30, 2015

FUNDI mwashi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti ndugu yake



FUNDI mwashi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti ndugu yake Pingu 
FUNDI mwashi, Lazaro Damian (18) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti ndugu yake.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na ilisomwa na Hakimu Flora Mjaya. Hakimu Mjaya alisema kwamba upande wa mashitaka ulithibitisha mashitaka yake bila ya kuacha shaka, kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Alisema kwamba kupitia kwa mashahidi wanne waliotoa ushahidi wao na vielelezo, ikiwamo hati ya Polisi ya matibabu (Pf3), vimeithibitishia Mahakama hiyo hadi kumtia hatiani mshitakiwa huyo.

"Mahakama imemtia hatiani kwa kosa la kulawiti, hivyo na kuhukumu kifungo cha miaka 30 jela,'' alisema Mjaya. 

Awali, Wakili wa Serikali, Munde Kalombola alidai kwamba kutokana na kuongezeka na matukio ya kulawitiwa kwa watoto wadogo, mshitakiwa apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.

Kabla ya hukumu, aliiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kumfunga kifungo cha nje kwa kuwa hana wazazi na kwamba amekaa rumande muda mrefu.

Ilidaiwa siku isiyofahamika Mei mwaka jana, maeneo ya Chanika, Dar es Salaam, Damian alimlawiti mtoto wa kiume ambaye ni mjomba wake, kinyume cha sheria ya nchi.