Friday, January 30, 2015

BIBI ANAYEDHANIWA KUWA MCHAWI AKUTWA AKIWA UCHI HUKO MAGEUZI MJINI SHINYANGA



BIBI ANAYEDHANIWA KUWA MCHAWI AKUTWA AKIWA UCHI HUKO MAGEUZI MJINI SHINYANGA

Bibi(aliyeko pichani) ambaye hajulikani jina wala anakotoka na ndiyo huyo amezua kizaa zaa baada ya kukutwa nje ya nyumba ya mkazi wa mtaa huo aitwaye Suzana Mwandu akiwa uchi wa mnyama hajitambui huku akitembea kwa kutumia makalio yake.Baada ya kukutwa akiwa uchi wasamaria wema waliamua kumvalisha nguo kusitiri mwili ingawa bibi huyo alijaribu kuzivua lakini baadaye kutulia na kuanza kuzungumza maneno yasiyoeleweka
Hapa ni katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi mjini Shinyanga pichani ni wakazi wa Ndembezi wakishuhudia tukio hilo la aina yake limevuta hisia za wakazi wa kata ya Ndembezi huku wengine wakidai kuwa bibi huyo ni mchawi kutokana na kiburi alichokuwa nacho huku akidiriki kupiga watu na kwamba mikono yake inaonekana imekatwa panga na imekomaa sana ambapo wataalamu wa mambo walisema huenda bibi huyo huwa anajigeuza Fisi na kutembelea mikono
Mwonekano wa mikono ya bibi huyo iliyoonekana kama imekatwa kwa mapanga na imekomaa kwa nyuma
Malunde1 blog iliyofika eneo la tukio haraka iwezekanavyo kama kawaida yake imeambiwa kuwa bibi huyo ambaye hakujulikana jina wala makazi yake awali alikuwa haongei na aliposemeshwa ndipo akaanza kuongea kwa lugha ya Kisukuma maneno yasiyoeleweka huku akisikika akisema wenzake wamemuacha alikuwa anaenda kwenye sherehe
Hatimaye bibi akaweza kusimama na kuanza kufanya vituko vya kila aina
Bibi akaamua kukaa na kuanza kutoa pesa alizokuwa amezifunga kiunoni kwa kwenye mfuko wa rambo laini uliokuwa umefungwa kitaalam
Bibi akiangalia pesa zake
Zilikuwa ni shilingi za hamsini hamsini,mia moja ,mia mbili,mia tano na elfu akaziweka kwenye kibakuli kilichokuwa eneo la tukio

Kushoto ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi Waziri Musa(CHADEMA) akisaidiana na wananchi wa eneo hilo kumwondoa bibi huyo kwenye nyumba ya mkazi wa eneo hilo

Bibi akawekwa chini ya mti,hata hivyo akaendelea kufanya vituko na kuamua kulala juu ya mawe,angalia hapa chini
Bibi akiwa amelala juu ya mawe kabla askari polisi hawajafika eneo la tukio leo mchana japokuwa bibi huyo amekutwa nyumbani kwa mtu saa moja asubuhi-picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Askari polisi wakimwangalia bibi huyo
Askari polisi wakitoa maelekezo kwa wananchi wa mtaa huo ambapo walisema serikali haiamini ushirikina hivyo kuwataka wananchi waondoke eneo la tukio na kumwacha bibi aendelee na safari yake kwani tayari alikuwa amepata nguvu na kuanza kutembea kwa miguu badala ya makalio kama mwanzo
Askari polisi akiwa amembeba bibi huyo kumtoa kwenye mawe,na katika hali ya kushangaza bibi huyo alimng'ang'ania askari huyo.Mpaka malundeq blog inaondoka eneo la tukio saa 14:10pm wakazi wa Mageuzi walikuwa wameanza kutawanyika huku bibi huyo akiondoka katika mtaa huo