Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na washiriki wa hafla ya kuwakumbuka walinzi wa amani wakisimama kwa dakika moja kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti mwaka 2010 na wale ambao wamepoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014.
Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo iliibua hisia na majonzi makubwa miongoni wa washiriki wa hafla hiyo ya kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza wajibu wao wa kuwasaidia wananchi waliokuwa matatizoni. Miongoni mwa wahanga hao waliokumbukwa katika hafla hiyo ni Mashuja Watatu Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) waliopoteza maisha wakati wakitimiza wajibu wao katika Misheni ya Kulinda Amani ya MONUSCO katika Jamhuri ya Kidemokraria ya Kongo. Mashujaa hao ni Luteni Rajabu Mlima, Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akitoa heshima zake mbele ya mshumaa mkubwa ambao uliandaliwa kama ishara ya kuwakumbuka na kuwaenzi Walinzi wa Amani na Watoa Misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao katika kipindi cha tetemeko la aridhi lililotokea mwaka 2010 huko Haiti na wale waliopoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. katika kipindi hicho Tanzania ilipoteza mashujaa wake watatu waliokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO huko DRC.
Na Mwandishi Maalum
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akitoa heshima zake mbele ya mshumaa mkubwa ambao uliandaliwa kama ishara ya kuwakumbuka na kuwaenzi Walinzi wa Amani na Watoa Misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao katika kipindi cha tetemeko la aridhi lililotokea mwaka 2010 huko Haiti na wale waliopoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. katika kipindi hicho Tanzania ilipoteza mashujaa wake watatu waliokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO huko DRC.
Na Mwandishi Maalum
Umoja wa Mataifa jana Alhamisi umewakumbuka walinzi wa Amani na wafanyakazi ya umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yako katika kipindi cha Octoba 2013 na November 2014.
Kumbukumbuka hiyo imefanyika katika siku kama ya jana ( January 8) miaka mitano iliyopita palitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti na kupoteza maisha ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo pamoja na uhalibifu mkubwa wa mali ilivuta hisia za waliohudhuria hata baadhi yao kutokwa na machozi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akizungumza katika hafla hiyo amesema, anasikitishwa sana na ongezeko la mashambulizi yanayofanywa dhidi ya walinzi wa Amani pamoja na watoaji wa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Jumla ya wahanga 102 walipoteza maisha nchi Haiti wakati lilipotokea tetemeko hilo mwaka 2010, huku wengine 100 walipoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. Wahanga hao ni walinzi wa Amani na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka mataifa mbalimbali duniani na walikuwa wakihudumu katika Misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa na Mashirika yake.
Kati ya waliokumbukwa jana wapo walinzi wa Amani watatu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walipoteza maisha huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO.
Mashujaa hao wa kitanzania na ambao majina yao yalisomwa moja baada ya jingine sambamba na mashujaa wenzao wengine. Ni Luteni Rajabu Mlima, Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila.
Ban Ki Moon amesema walinzi wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu wamekuwa wakipoteza maisha katika mazingira ambayo ukiacha yale yatokanayo ya majanga asili yakiwamo magonjwa ya milipuko na ajali, wengine wamepoteza maisha kwa mashambulizi yanayofanywa kwa makusudi.
Na kwa sababu hiyo Katibu Mkuu anasema, Umoja wa Mataifa unaendelea na jitihada zake za kuimarisha ulinzi wao ikiwa ni pamoja na kuwajengea mazingira salama ya utendaji kazi yakiwamo mafunzo na vifaa
Ameongeza kuwa ushirikiano na michango kutoka nchi wanachama wa umoja wa mataifa ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambapo siyo tu pamekuwapo na ongezeko kubwa la mahitaji ya walinzi wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu, lakini pia kutokana na ongezeko la mashambulizi dhidi yao na mazingira magumu ya kazi.