kamishna wa uhamiaji na usimamazi na uthibiti wa mipaka Abdallah Khamis akipata maelekezo kutoka kwa maofisa wa uhamiaji namna zoezi la kuandikisha raia wa kigeni linavyofanyika.
Maofisa wa uhamiaji wakichukua alama za vidole
Moja ya kitambulisho wanachopewa Raia wasio wa Tanzania .
Raia wa Congo ambaye ameishi nchini isivyo halali kwa miaka kumi na moja akifurahi na familia yake baada ya kupata vitambulisho vya kuishi nchini kihalali.
Baadhi ya wananchi ambao si raia wa Tanzania ambawaliojitokeza katika zoezi la kuandikishwa ndani ya uwanja wa Lkae Tanganyika
Na Editha Karlo,wa Blog ya Jamii,Kigoma.
IDARA ya uhamiaji kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la uhamiaji(IOM) wamezindua zoezi la kuandikisha raia wote wa kigeni wanaoishi nchini isivyo kihalali.
Kamishna wa uhamiaji Abdallah Khamis, anayeshughulikia usimamizi na uthibiti wa mipaka akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika viwanja vya Lake Tanganyika ,alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuwatambua raia wote wasio Watanzania na kuwapa hadhi ya inayostahili na hili ni zoezi la nchini nzima limeanza Kigoma litaendelea na mikoa yote ya Tanzania.
''Kuna raia wakigeni hawana sifa za kuishi nchini ila tayari wamelowea huku na wameishi miaka mingi,na pia wapo wanaoishi nchini kwa vile wameolewa au wameoa Watanzania,kwakweli zoezi hili litasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa utata ambao umekuwepo kwa muda mrefu wa nani raia na nani si Raia wa Tanzania''alisema Kamishna Abdallah
Kamishna huyo alisema pia zoezi hilo halina uhusiano wowote na uchuguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani pamoja na uchaguzi wa serekali za mitaa.
''Hii itasaidia sana kuondoa wahamiaji haramu waliokuwa wakijiingiza katika masuala ya siasa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kitu ambacho si sahihi''alisema Kamishna
Naye Ofisa uhamiaji wa Mkoa wa Kigoma Ebrossy Mwanguku alisema kuwa lengo hasa la zoezi hilo pia ni kuondoa raia kutoka nje ya nchi wanaoishi nchini bila ya kuwa na vibali halali vya kuishi nchini.
Alisema kuwa sehemu kubwa ya wahamiaji waliojitokeza katika zoezi hilo ni raia kutoka nchi za Burundi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC)Uganda na Rwanda.
Aliwataka Raia wote wanaoishi nchini isivyo halali kujitokeza katika zoezi hilo kwani baada ya kukamilika kwa zoezi hilo desemba 21 kwa Mkoa wa Kigoma yeyote atakaye kamatwa sheria zitachukua mkondo wake.
Kiongozi wa shirika la IOM Tamara Keating alisema kuwa hayo ni matokeo ya oparesheni kimbunga iliyobaini kuwepo nchini kwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu,