Tuesday, December 16, 2014

WAZIRI MAKALA AWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WEZI WA MAJI



WAZIRI MAKALA AWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WEZI WA MAJI
SAM_0190Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiongea na vyombo vya habaria katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
SAM_0188
 Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga
SAM_0178

Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
SAM_0191
Askari anayelinda eneo hilo

SAM_0183Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala wa nne kulia akiwa anateta jambo katika moja ya maporomoko ya maji ijulikanayo kama mto nduruma wengine ni watumishi wa mamlaka hiyo.
SAM_0173Kulia aliyesimama ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya maji Mkoa wa Arusha Bw.Joshua Kileo akiwa anazungumza wakati Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala alipokuwa anazungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Arusha leo
SAM_0208Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiwa anaangalia moja ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji katika eneo la kisongo ambacho kitasaidia wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya maji
SAM_0201Hii ni mitambo ya kuwekea maji dawa
SAM_0200Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiangalia moja ya kisima cha maji katika kijiji cha Olturuto wilaya Arumeru
SAM_0205Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akionge akatika moja ya chanzo cha maji kinachotengenezwa eno la kisongo Mkoa Arusha

Na Pamela Mollel wa jamiiblog.


Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuwafichua wale wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.Alitoa wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji

Waziri Makala alisema kuwa serikali inafanya jitihada ya kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na kuboresha miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa wananchi."Wizi wa kujiunganishia maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni ya kuwasaka wale wote wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria"alisema Makala

Aidha katika moja ya chanzo kikubwa cha maji mto nduruma alisema kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi kwa mamlaka ya maji kwa kuwa wabunifu.
Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni walikuwa na zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kufanikiwa kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo bado ni endelevu