Saturday, December 06, 2014

Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakutana Arusha kujadili Sera ya Vijana wa EAC



Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakutana Arusha kujadili Sera ya Vijana wa EAC
 Mbunge kutoka Kenya Mhe. David Ocheng akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.
 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Jesca Eriyo (kushoto) akitoa mada wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania. Kulia ni mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.

 Mmoja wa vijana kutoka Uganda Bi. Helena Okiring akichangia wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.
 Bi. Stella Massekwe kutoka Uganda akitoa mchango wake kuhusu masuala mbalimbali yaliyozungumzwa wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania, Kushoto ni kijana Baraka Chelego kutoka Tanzania.
Baadhi ya Vijana kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Tanzania bara na visiwani, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wakifuatilia matukio yaliyokua yanaendelea wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.



Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo.