Tuesday, December 09, 2014

Umoja wa Mataifa unasema kua zaidi ya watu milioni tatu wanahitaji msaada wa dhahura kwa sababu ya tatizo kubwa la utapia mlo na mgogoro



Umoja wa Mataifa unasema kua zaidi ya watu milioni tatu wanahitaji msaada wa dhahura kwa sababu ya tatizo kubwa la utapia mlo na mgogoro

Tahadhari hio imetolewa miaka mitatu baada ya zaidi ya robo ya watu milioni moja kufariki kutokana na ukosefu wa chakula.

Katika taarifa yake ofisi ya mratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa inasma kuwa wasomali wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu
ya kibindamau.

Ukame na uhaba wa chakula limekuwa tatizo kwa wengi Somalia inayokumbwa na vita Maelfu ya watu wameathirika kutokana na vita vinavyosababishwa na wanamgambo wa Al Shabaab.

Kikosi cha wanjeshi wa Muungano wa Afrika kiko nchini humo kuoambana na wanamgambo hao.

Wadadisi wanasema hali hiyo imechocewa zaidi na ukame pamoja na mafuriko katika baadhi ya
sehemu za nchi hio.