Mamlaka ya Usafirishaji Tanzania (SUMATRA) imeanza ukaguzi wa nauli katika vyombo vya usafirishaji hapa nchini hasa kwenye mabasi ya abiria yaendayo mikoani kutokea jijini Dar es salaam.
SUMATRA imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa kuna baadhi ya vyombo vya usafiri hasa mabasi ya Mikoani kuwa na tabia ya kuongeza nauli hasa katika kipindi hiki cha msimu sikukuu za Krismas na Mwaka mpya,ambapo mapema leo asubuhi maafisa wa Mamlaka ya Usafirishaji Tanzania (SUMATRA) walitia timu katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar na kuanza kazi ya Ukaguzi huo kwa kuangalia tiketi ya kila abiria na hapo ndipo walipobaini kuwa kweli kuna abiria wengine wameuziwa tiketi kwa bei ya juu kuliko ile iliyopangwa.
Abiria wote waliotozwa nauli kubwa walirudishiwa nauni zao na wahusika wa mabasi hayo walipewa onyo kali la kutofanya hivyo tena na kutozwa faini kwa kosa hilo.
Zoezi hilo la ukaguzi lipo katika maeneo yote hapa nchini na zoezi litadumu kwa kipindi chote.
viwango vya nauli za mikoani.