KAMPUNI ya Scania nchini Tanzania imekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanya biashara wa mabasi ya abiria pamoja na wafanya biashaya ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya abiri kutoka makampuni mbalimbali wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Chesisi za Scania yaliyoandaliwa na Kampuni ya Scania yaliyojulikana kama " Scania Bus Expo" yaliyo fanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania, Godwin Rwegasira alisema leo ni siku ya kuwakumbusha wafanya biashara wa mabasi ya abiria na watengeneza mabodi kuwa watumie Chesisi za Scania kwa wale ambao hawajawahi na wale ambao wanatumia waendelee kutumia kwani ni bora,imara na zinadumu kwa muda mrefu na zaidi ya yote spea zake zinapatika mahali pote kwenye vituo vya Scania.
Alisema Rwegasira, Scania ni vumilivu sana inaweza kuhimili miundombini ya namna yeyote hususani barabara zetu za Afrika mashariki za vumbi, hivyo tutumie chesisi za Scania mkombozi kwa biashara yako ya mabasi ya abiria.
Nae Afisa mauzo kutoka Kampuni za kutengeneza mabodi ya mabasi ya Master kwa niaba ya watengeneza mabodi kutoka makampuni mbalimbali alisema Chesisi za Scania ni bora, zina zinahimili shida, ni imara na spea zake zinapatikana hivyo kwa niaba ya watengeneza mabodi alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia Chesisi za Scania katika biashara zao za mabasi ya abairia.
Makampuni mabalimbali ndani nan je ya nchi yalialikwa katika maonyesho hayo ambayo ni Master Fabricator kutoka Kenya, Dar Coch kutoka Tanzania, Choda kutoka Kenya, LSHS kutoka Tanzania, Quality Garage kutoka Tanzania, Stanbic Bank na Scania Finance pamoja na wafanyabishara wa mabasi ya abiria.
Meneja Mauzo na masoko wa kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya abiria ya Choda kutoka Kenya, Pius Wambua(kulia) akiwaonyesha wageni waalikwa baadhi mabasi waliyowahi kutengenezwa na kampuni hiyo katika picha wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Scania yaliyojulikana kama "Scania Bus Expo" yenye malengo ya kuhamasisha wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kutumia Chesisi za Scaina.Maonyesho yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha Ubungo Dar es Salaam.
Meneja mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania, Godwin Rwegasira(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Chesisi za Scania yaliyojulikana kwa "Scania Bus Expo" yenye malengo la kuwahamasisha wafanya biashara wa mabasi ya abaria kutumia chesisi za Scania kutokana na ubora wake.Maonyesho hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni watengeneza mabodi wa mabasi ya Abiria, Pius Wambua meneja mauzo na masoko kutoka kampuni ya Choda Kenya(kushoto) na Peter Gitau Afisa mauzo ktoka kampuni ya Masters kutoka Kenya.
Afisa masoko wa kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya, Master kutoka Kenya, Peter Gitau(kushoto) akiwaonyesha wageni waalikwa baadhi mabasi waliyowahi kutengenezwa na kampuni hiyo katika picha wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Scania yaliyojulikana kwa "Scania Bus Expo" yenye malengo ya kuhamasisha wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kutumia Chesisi za Scaina.Maonyesho yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha Ubungo Dar es Salaam.