Kaimu Mwenyekiti wa umoja wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi(TAMONGSCO),Bw.Leonard Mao(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maamuzi ya Serikali kutatua mgogoro wa TAMONGCO,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo,Bw.Mrinde K.Mnzava.
Na Bakari Issa,Dar es Salaam.
Uongozi wa shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali(TAMONGSCO) lililokuwa katika mgogoro na kikundi cha waliokuwa viongozi wa kitaifa(National Office Bearers) kilichofanya hujuma za kutaka kuifanya TAMONGSCO kuwa mali yao binafsi.
Mara baada ya Katiba kufanyiwa marekebisho kumi(10) na mkutano mkuu(AGM) uliofanyika Mbeya katika ukumbi wa Benjamin William Mkapa,AGM iliagiza kamati kuu ya Taifa (NEC) kuingiza marekebisho hayo kwenye katiba na kuipeleka kwa msajili wa asasi za kiraia(CSO) ambaye ni Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi.
Akithibitisha uongozi wa shirikisho hilo,Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali,Bw.Leonard Mao amesema uongozi uliokuwa madarakani ndiyo sahihi pamoja na Katiba iliyopita na kuongeza kuwa wanaosema katiba na uongozi uliochaguliwa sio sahihi hao sio wanachama wetu na kuagiza waache kabisa.
âUongozi wa waliotaka kuchakachua katiba ya umoja huu,muda wao umekwisha na uongozi uliochaguliwa ndio uongozi sahihi pamoja na katiba iliyopendekezwa,na wanaosema uongozi pamoja na katiba iliyopendekezwa sio halali hao si wanachama wetu na waache kabisaâ,alisema Bw.Mao
Naye Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo,Bw.Mrinde Mnzava alisema kuwa umoja huo ndiyo unaoongoza kutoa wanafunzi bora nchini na kuisaidia Serikali kuweka vizuri miundombinu ya shule pamoja na vyuo.
Aidha amesema umoja huo utafanya kikao mkoani Dodoma ili kuteua nafasi ya Mwenyekiti ambayo imeachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti Kitaifa,Ally Hassan Mwanakatwe aliyefariki dunia.
âUmoja huu unalisaidia Taifa katika kutoa wanafunzi bora na kuipa changamoto Serikali kuboresha miundombinu ya shule na vyuo kwa ujumla na tunatarajia kufanya kikao mkoani Dodoma ili kumchagua Mwenyekiti mpya kitaifaâ,alieleza Mnzava
Pia Naibu Katibu Mkuu wa TAMONGSCO,Bw.Chelestino Mofuga alitoa pongezi kwa Serikali kwa kuweza kusuruhisha suala hilo ambalo kwa sasa limefika mwisho na kuhakikisha kuwa mgogoro huo haupo tena.
âPongezi kwa Serikali kwa suala hili,lakini wamiliki wa shule binafsi tunakabiliwa na changamoto ya lugha katika kufundishia katika shule pamoja na vyuoâ,alimaliza kusema Mofuga