Friday, December 05, 2014

Mahafali DIT kufanyika Januari 2015



Mahafali DIT kufanyika Januari 2015
Mahafali ya nane ya Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika Januari 31 mwaka huu katika viwanja vya chuo hicho na yatatanguliwa na utoaji wa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wahitimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao. 

 Taarifa ya DIT kwa vyombo vya habari imesema kuwa tuzo kwa wanafunzi zitatolewa Januari 23 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya mahafali hayo ambayo wahitimu katika ngazi na masomo tofauti watatunukiwa. Wahitimu watakaotunukiwa ni siku hiyo ni pamoja na wa Stashahada ya Uhandisi (Ordinary Diploma), cheti cha awali cha TEHAMA (IT) mwaka wa masomo 2013/2014.

 Wahitimu wametakiwa kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki mahafali hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz na "Rehearsal" itafanyika Ijumaa tarehe 30 Januari 2015. 

 "Malipo ya Tshs 30,000/= kwa ajili usajili yatafanyika kwenye tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.ac.dit.tz" Inasema taarifa hiyo. Malipo yanatakiwa klufanyika kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu iliyotolewa kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na dhumuni la malipo mf. 

Ada, transcript na graduation. Kulingana na taarifa hiyo, mwisho wa kujisajili ni tarehe 31 Desemba, 2014 na wahitimu wametakiwa kufahamisha kuhusiana na mahafali hayo.