Saturday, December 20, 2014

KWIECO YATOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI KILIMANJARO...

Afisa Habari wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mkoani Kilimanjaro (KWIECO), Veronica Ollomi akifafanua jambo katika Warsha ya siku mbili kwa waandishi wa Habari  wa mkoa wa Kilimanjaro, kilichofanyika juzi mjini Moshi, kwa lengo la kuwapa mafunzo juu ya Haki za Binadamu na Sheria zake. 

 Washiriki wa Warsha ya Haki za Binadamu, waandishi wa Habari mkoani Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo, yakiwemo swala la Wosia, Sheria ya Ardhi kwa Lengo la kuwawezesha kupata uelewa wa sheria hizo katika utendaji wao wa kazi.
 Mtangazaji wa Redio Moshi FM, Neema Mkotya akiweka sawa mitambo kabla ya kuwasilisha Mada. 
 Mtaalamu wa maswala ya Haki za Binadamu kutoka KWIECO, Elizabeth Mushi akifafanua jambo kwa washiriki wa Warsha hiyo.
 Waandishi wa Habari, Heckton Chuwa (Bussiness times), Nakajumo James (Habari Leo) na Happiness Tesha (Raia Tanzania) wakifuatilia mafunzo.


Sehemu ya Washiriki wa Warsha ya Haki za Binadamu, Waandishi wa Habari wa mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia uwasilishaji wa Mada katika Warsha hiyo.


Mwezeshaji Elizabeth Mushi akiendelea na Uwasilishaji wa Mada mbalimbali katika Warsha hiyo

Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Johnson Jabir, akiwasilisha kazi iliyofanywa na kundi lake kwa niaba ya wenzake. 


Na Dixon Busagaga wa Globu ya 

Jamii Kanda ya Kaskazini