Monday, November 10, 2014

WAZIRI MIGIRO AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA HOTELI YA MALAIKA JIJINI MWANZA



WAZIRI MIGIRO AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA HOTELI YA MALAIKA JIJINI MWANZA
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro, WAZIRI wa Katiba na Sheria akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Majaji katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza,Maudhui ya Mkutano huo ni kujitathmini Kama njia bora ya kuboresha Mahakama. Mhe. WAZIRI amefungua Mkutano huo kwa niaba ya Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akitoa Mada katika Mkutano wa Majaji unaofanyika mkoani Mwanza.
Mhe. Jaji Sauda Mjasiri, Jaji wa Mahakama ya Rufani, (aliyeketi mbele, wa kwanza kushoto), Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar (wa kwanza kulia) pamoja na Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) wakiwa pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Mahakama ya Tanzania wanaohudhuria katika Mkutano huo. 
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro, Waziri wa Katiba na Sheria (wa nne kushoto), Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa tatu kushoto), Mhe. January Msoffe, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa pili kushoto), Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar, (wa pili kulia), Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa kwanza kushoto) pamoja na Mhe. Jaji Mwangesi, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa ni baadhi ya Majaji wote waliohidhuria katika Mkutano huo Mkuu wa mwaka unaofanyika jijini Mwanza.(Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).