Thursday, November 20, 2014

WANAFUNZI ST.JOHNS DODOMA WAGOMA MPAKA KIELEWEKE



WANAFUNZI ST.JOHNS DODOMA WAGOMA MPAKA KIELEWEKE
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo kikuu cha St Johns Manispaa ya Dodoma Danny Damian akiwahutubia wenzake, kwenye uwanja wa michezo wa Chuo hicho leo Jumatano Novemba 19, 2014. Wanafunzi hao wametangaza mgomo wa kutoingia madarasani hadi hapo kero zao zote zitakaposhughulikiwa na uongozi, kubwa kuliko zote ni uhaba wa walimu na hata wale waliopo uwezo wao wa kufundisha haukidhi viwango. Wanafunzi hao wameenda mbali zaidi na kuutaka uongozi wa chuo hicho kilicho chini ya kanisa moja hapa nchini, kukirudisha serikalini kama "Ngoma" imewashinda
Huu ni umati wa wanafunzi hao wakimsikilkiza rais wao