Thursday, November 20, 2014

CHINGAS WALIVYOPAMBANA NA POLISI JIJINI MWANZA



CHINGAS WALIVYOPAMBANA NA POLISI JIJINI MWANZA
Polisi wa kutuliza ghasia, wakifanya doria kwenye mitaa ya jiji la Mwanza baada ya kutokea ghasia kufuatia askari wa jiji hilo kufanya jaribio la kuwaondoa wamachinga kwenye soko kuu, rwagasore na mtaa wa Lumumba mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014
Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa wamejihami kwa silaha wakati wakituliza ghasia za wamachinga kwenye mitaa ya jiji hilo mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014. Zogo hilo lilizuka baada ya askari wa jiji walipowavamia wamachinga na kuwaamuru waondoke kwenye maeneo ya soko kuu, Rwagasore na mtaa wa Lumumba na hapo ndipo "Kasheshe" lilipozuka ambapo askari wa jiji walizidiwa nguvu kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wamachinga mithili ya maroketi na kuwafanya warudi nhyuma na ndipo polisi wa kutuliza ghasia walipoitwa na kuwakabili wamachinga hao.
Moja ya barabara za jiji la Mwanza ikionekana kuwa nyeupe huku watu wachache wakitafuta mahala salama baada ya polisi kupambana na wamachinga mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014
Machinga, akirusha jiwe, wakati polisi wa kutuliza ghasia walipoingia mtaani na kupambana na wafanyabiashara ndogondogo jijini Mwanza maarufu kama wamachinga, leo Jumatano Novemba 19, 2014