Monday, November 10, 2014

WANAFUNZI 48 WA CHUO CHA KILIMO NICE DREAM WATELEKEZWA SIKU TANO BILA YA CHAKULA NA CHUO HAKIJASAJIRIWA MBEYA




WANAFUNZI 48 WA CHUO CHA KILIMO NICE DREAM WATELEKEZWA SIKU TANO BILA YA CHAKULA NA CHUO HAKIJASAJIRIWA MBEYA
Chuo hiki kilizinduliwa mwaka huu na Mh .Frederick Sumaye Waziri mkuu Mstaafu


Moja kati ya mwanachuo aliyezirai kwa njaa akiinuliwa na wasamaria wema kwenda mpatia chakula

Moja kati ya mabweni ya chuo hicho ambapo hulala chini wanafunzi kati ya 10 mapaka 15 kweli taasisi zinazihusika na ukaguzi wa vyuo hivi zipooo?


Hapa wanachuo hao wakipata uji baada ya msamaria mwema kuwapatia uji huo

Wakipata chakula cha mchana baada ya wananchi wa ilemi kuchangia chakula

Baadhi ya wanachama wa chadema walifanikiwa kuchangishana na kuapata debe 7 za mahindi na fedha taslimu  sh 20,000/


Hii ndilo shamba darasa la chuo hicho


Wanachuo 48 wa Chuo cha Kilimo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini Mbeya wanakabiliwa na ukosefu wa chakula baada ya uongozi wa Chuo hicho kuwatelekeza na wao kutokomea kusikojulikana.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Ilemi Mheshiwa Furaha Mwandalima baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachuo hao na kufika Chuoni hapo na kujionea hali halisi.

Mwandalima alichukua hatua za haraka za kumtafuta Mstahiki Meya ambaye alimshauri kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wilila ya Mbeya ili kupata mustakabali wa suala hilo.

Hata hivyo lilitolewa agizo la kuorodhesha majina ya wanafunzi na mahali wanakotoka ili kuwarudisha makwao na Chuo kifungwe kutokana na Chuo hicho kutosajiliwa rasmi na kwamba kilikuwa kinaendeshwa kijanja na wanachuo hao wamelipa malipo ya awli zaidi ya shilingi laki tano.

Zaidi ya wanafunzi 40 wanatokea Mkoa wa Kagera na wawili wakitokea mkoani Mara ambapo wawili wanatokea wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya hali mmoja akitokea Mkoa wa Dar es Salaam.

Mmoja wa wanachuo aliyejitambulisha kwa jina la Jenitha Carist alisema waliletewa taarifa na wakuu wa shule walizokuwa wakisoma baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka uliopita kuwa wamechaguliwa na serikali kusomea Kilimo Mkoani Mbeya lakini walipofika walishangazwa na hali waliyoikuta na kwamba walipofuatila kwenye mtandao walibaini chuo kutosajiliwa katika Baraza la Vyuo.

Walipoutafuta uongozi wa Chuo hicho ulianza kupiga chenga ndipo walikwenda kutoa taarifa Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo uongozi wa Wilaya umeanza hatua za kumtafuta mmiliki ili aweze kutoa majawabu.

Hali ilikuwa tete siku ya Jumamosi ambapo baadhi ya wanachuo walizirai kwa njaa na kulazimu Diwani Furaha Mwandalima kufanya changizo la dharula na kufanikiwa kukusanya debe nne za mahindi na maharage debe moja na kuandaa chakula cha dharula nakuwaandalia mlo wa mchana.

Baadhi ya majirani walishindwa kujizuia kwa kuangua kilio kutokana na hali mbaya kwa baadhi ya wanachuo ambapo baadhi walilazimika kuandaa uji ili kutoa msaada wa haraka.

Kwa upande wake Diwani Mwandalima amemshukuru Mstahiki Meya Athanas Kapunga na Mkurugenzi kwa kuhudi zao ili kuwafanya wanachuo hao wafarijike hasa kutokana na wengi wao kutokuwa na na ndugu na wanatoka mikoa ya mbali.

Mwandalima ametoa wito kwa wakazi wa Mbeya kutoa mchango wa hali na mali ili kuokoa maisha ya wanachuo hao pia amewashukuru wakazi wa Ilemi kwa kuchangia chakula na mahitaji mengine kwa wanachuo hao.

JE MNAOHUSIKA KUSAJIRI VYUO HIVI MPO? AU MKEKAA TU MAOFISINI KUPIGA SOGA KUSUBIRI MSHAHARA TU MAANA MBEYA KILA KUKICHA VYUO VINAZINDULIWA  HEBU WAONEENI HURUMA WAZAZI WANAVYOTABIKA KUITAFUTA ADA KWA AJILI YA WATOTO WAO NA MWISHO WANAAMBIWA CHUO HAKIJASAJIRIWA MWEEE

TAOA MAONI YAKO JUU YA UTAPELI HUU WA VYUO  AMBAVYO HAVIJASAJIRIWA


Na Mbeya yetu