Tuesday, November 18, 2014

Vodacom yaja na promosheni ya “shinda na kabumbu”



Vodacom yaja na promosheni ya "shinda na kabumbu"
Wadau wa soka nchini na wateja Vodacom Tanzania kwa ujumla wameletewa Promosheni mpya na ya aina yake iliyozinduliwa jana na kampuni hiyo ambapo imewalenga wapenzi wa soka na wateja wa kampuni hiyo kushiriki katika Promosheni ya "SHINDA NA KAMBUMBU"

Promosheni hii ambayo itadumu kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo itawafanya wapenzi wa soka kuchemsha bongo kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Ligi kuu ya Uingereza,na masuala mengine mengi yanayohusiana na Kombe la Dunia na mengine mengi yanayohusiana na mchezo wa soka kwa ujumla.

Kila siku wapenzi wa soka au wateja 5 watajinyakulia shilingi 50,000 pia atakuwepo mshindi mmoja wa wiki atakaejinyakulia shilingi Milioni 1. Na droo ya mwisho katika promosheni hii tutapata mshindi wa jumla atakaejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 pesa taslimu. Ili kushiriki katika promosheni hii mpenzi wa soka au mteja yeyote wa mtandao huu anachopaswa kufanya ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 na hapo mteja atakatwa kiasi cha shilingi 99 tu kwa kila meseji.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hii Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amewasihi wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla kushiriki katika promosheni hii na kutuma meseji nyingi za kujibu maswali yanayohusiana na soka ili waweze kujishindia zawadi na kufanya maisha yao kuwa murua.

"Wakati umefika tena kwa wateja wa Vodacom na wapenzi wa mpira wa miguu kujishindia zawadi kemkem kupitia promosheni hii kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote,na kupitia promosheni mbalimbali za kampuni hii wateja wetu wengi wameweza kunufaika na maisha yao kuwa murua kwa kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu".Alisema Nkurlu.

Amesema kila wiki washindi watakuwa wakitangazwa na kupigiwa simu moja kwa moja baada ya kufanyika droo za kila wiki na kutumiwa fedha zao kwa njia ya M pesa na alitumia nafasi hiyo kuwapa tahadhari na matapeli ambao wamekuwa wakitumia promosheni kama hizi kuwarubuni wateja kuwa wawatumie fedha ili waweze kushinda zawadi wakati hawahusiki na promosheni hii.

Vodacom imekuwa ikiandaa promosheni mbalimbali kwa wateja wake na moja ya promosheni ambayo imewafanya wateja wake maisha yao kuwa murua ni ile ya Timka na bodaboda na Vodacom milionea ambapo washindi waliweza kujishindia pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 100.
001&002.Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya "SHINDA NA KABUMBU"inayolenga kuwawezesha wadau wa soka na wateja wa kampuni hiyo kushiriki kwa kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 ambapo mteja atakuwa akiulizwa maswali mbalimbali kwa njia ya ujumbe kuhusiana na maswala ya soka na kuweza kujishindia fedha taslimu kuanzia shingili elfu 50 mpaka Milioni 5/= kulia ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe,hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.