Sunday, November 23, 2014

Taswira mbali mbali za Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (AGF)



Taswira mbali mbali za Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (AGF)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa tatu kutoka kushoto) akizindua Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 20 Novemba 2014. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sammy Mollel (kulia).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (kushoto) akihutubia wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, washiriki (exhibitors) na wanunuzi wa madini ya vito ambao wamehudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yanayofanyika jijini humo kuanzia tarehe 18 hadi 20 Novemba, 2014.
Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,wakifuatilia majadiliano uendelezaji endelevu wa madini ya Tanzanite nchini. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, John Nayopa, Kamishna Msadizi wa Madini-Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane, na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara, nchini Thailand, Tony Brooks akionesha machapisho mbalimbali kuhusu madini ya Vito kwa mgeni rasmi wa maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kushoto), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa kwanza kutoka kushoto). Nchi ya Thailand ina uzoefu mkubwa katika uandaaji wa maonesho ya Vito ambapo wameshafanya maonesho zaidi ya 50 na wafanyabiashara wa madini ya Vito kutoka Tanzania wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo.
Wachimbaji wadogo wa madini ya vito kutoka ukanda wa Umba mkoani Tanga waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha wakiwa kwenye banda wanalouzia madini hayo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Pamoja nao ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Tanga, Mjiolojia Elias Kayandabila (wa nne kutoka kushoto).
Watendaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bruno Mteta, (wa pili kutoka kulia), Meneja Mipango na Utafiti, Julius Moshi (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Eng. Yisambi Shiwa (wa tatu kutoka kushoto) waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito Arusha, wakisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Eng. Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto) aliyetembelea banda la Wakala huo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Washiriki kutoka nchini Rwanda wakiwa na mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kulia), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa nne kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sammy Mollel, (wa nne kutoka kulia_mstari wa mbele).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa kwanza kulia) akizungumza na mfanyabiashara wa madini nchini, Peter Pereirra mara alipotembelea banda la mfanyabiashara huyo katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha. Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja.