Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abdu Jumaa iliyopo Kitunda, jijini Dar es Salaam, Enock Mseti (20) alitekwa na watu wasiojulikana kisha kuuawa kikatili na maiti yake kutupwa kando ya reli hivi karibuni.
"Mwanangu alikuwa afanye mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, ingawa kutokana na hali yangu kiuchumi kuwa mbaya, alikuwa amesimama kwenda shuleni, lakini nilikuwa katika jitihada za kuhakikisha anafanya mtihani huo," alisema mzee Mseti kwa huzuni.