Tuesday, November 11, 2014

SERIKALI YAKIFUNGA CHUO FEKI CHA KILIMO MBEYA



SERIKALI YAKIFUNGA CHUO FEKI CHA KILIMO MBEYA
Jamaa walivyo matapeli wametumia jina la Mh. Sumae Waziri mkuu mstaafu kuwa ndiyo alizinduo chuo hicho kumbe ni uongo mtupu
 Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala akitoa tamko la kufunga chuo hicho

Kulia ni Richard Mchomvu mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya akiwa na jalada la uchunguzi kuhusiana na chuo hicho

Baadhi ya wanafunzi wakiwa hawaamini tamko lililotolewa na Selikari juu ya kufungwa chuo chao



Hakika ilikuwa huzuni kubwa kwa wanachuo hao


Wakazi wa ilemi wakiomboleza na wanachuo hao




Serikal imekifunga chuo cha Kilimo na Mifugo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini na kuwataka wanachuo wa chuo hicho kuondoka chuoni hapo baada ya siku tatu.

Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala na kwamba Serikali itagharamia chakula kwa siku tatu ambapo Serikali ilikabidhi shilingi laki tatu kwa Mtendaji Kata Bi Gladness Sapuka kwa ajili ya kununua chakula kwa wanachuo 48 waliokuwa wakisoma katika chuo hicho ambacho hakina usajili kutoka Baraza la Vyuo(NACTE).

Tamko hilo lilamsha kilio chuoni hapo kutoka kwa wanachuo na wakazi wa Ilemi kutokana na wanachuo hao kutakiwa kuwasiliana na wazazi wao na walezi ili watumiwe nauli za kuwasafirisha makwao na wengi wao wakitokea mkoa wa Kagera na Mara na kwamba wanachuo hao wamekwisha lipa kila mmoja zaidi ya shilingi laki tano na elfu hasini.

Mbali ya chuo hicho kutosajiliwa na NACTE pia mmiliki wake hafahamiki vema na jalada la uchunguzi ili akamatwe kujibu tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia kivuli cha chuo na kuwatapeli wanachuo 48 waliokuwa na nia ya kusomea taaluma ya kilimo.

Kauli hiyo ilikuwa mwiba kwa wanachuo hao pale Kaimu Katibu Tawala aliposema kwamba Serikali haina chuo cha kuwapeleka kwa kuwa hakuna nafasi katka Vyuo vya Kilimo Mkoani Mbeya na muda wa usajili wa wanavyuo vya kilimo umemalizika.

Kaimu Katibu Tawala aliambatana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Richard Mchumvu ambaye alisema kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta mtuhumiwa na kwamba pindi atakapopatikana atafikishwa mahamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kwa upande wa wakazi wa Ilemi wameiomba Serikal kuangalia upya suala hilo kwa kuwa mtuhumiwa hajakamatwa hivyo serikali iwasaidie usafiri wa kuwaridisha wanachuo hao makwao ili kuwapunguzia makali kutokana na umbali wanaotoka.

Wazo hilo liliungwa mkono na Diwani wa Kata ya Ilemi Furaha Mwandalima ambaye alisema serikali ione hilo kama janga la moto au mafuriko il kuwasaidia kuwasafirisha makwao kwani wengi wa wanachuo hawana uwezo wa kupata nauli ya kuwafikisha makwao ambapo mwanachuo mmoja anahitaji kutumia zaidi ta shilingi laki moja na zaidi ya shilingi milioni sita zinahitajika kuwafikisha makwao.

Pamoja na kauli ya Serikali kutoa tamko wakazi wa Ilemi walibaki ili kujadiliana mustakabali wa wa wanachuo hao kutokana na wengi kutoka katika familia duni na wengi kuonekana kukata tamaa ya kuishi kwa kile walichodai kuwa mmoja wao alikuwa ni pacha na mwenzake ambapo nduguye aliozwa ndipo zikapatikana fedha za karo.

Na Mbeya yetu