Wednesday, November 26, 2014

Sekretarieti ya Maadili waendesha mafunzo ya Maadili kwa maafisa waandamizi wa Polisi Zanzibar



Sekretarieti ya Maadili waendesha mafunzo ya Maadili kwa maafisa waandamizi wa Polisi Zanzibar
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeendesha mafunzo ya Maadili kwa maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi walioko Zanzibar. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano ulioko katika Chuo cha Polisi mjini Zanzibar.

Mafunzo hayo yana lengo la kuwasaidia watendaji hao wa Jeshi la Polisi walioko Zanzibar kuweza kuondokana na changamoto nyingi za uvunjifu wa maadili ambazo watendaji hao wamekuwa wakikabiliana nazo.

Mafunzo hayo pia yana lengo la kuwakumbusha watendaji hao jinsi ya kuboresha na kuimarisha utendaji kazi ndani ya jeshi hilo huku wakizingatia maadili wakati wa utendaji kazi zao katika utumishi wa umma.

Akifungua mafunzo hayo Kwa niaba ya Kamishna wa Maadili, Mjumbe wa Baraza la Maadili Mhe. Hilda Gondwe aliwakumbusha watendaji hao wa Jeshi la Polisi Zanzibar na watendaji wengine kuwa wana wajibu mkubwa wa kulinda na kusimamia maadili ndani ya jeshi hilo ili kulinda imani ya wananchi kwa jeshi la polisi

Aliwataka watendaji hao kuzingatia maadili kwani kwa kufanya hivyo kutaimarsiha utawala bora nchini na kuimarisha utendaji kazi kwa ujumla na hivyo kuboresha utendaji kazi katika maeneo yao.

Mafunzo hayo yamewashirikisha watendaji waandamizi wa jeshi la polisi walioko Zanzibar kutoka katika mikoa mitatu ya kipolisi ya Kusini, Kaskazini na Mjini Magharibi kama OCD, RCO ambapo maafisa 35 walitarajiwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Katika mafunzo hayo jumla ya mada tatu za Sheria ya Maadili, Fomu ya Tamko la Mali na Madeni na Mgongano wa Maslahi ziliwasilishwa na wataalamu kutoka Sekretarieti ya Maadili
Mjumbe wa Baraza la Maadili Mhe.Hilda Gondwe akifungua rasmi mafunzo ya MAADILI kwa maafisa wa Polisi mjini Zanzibar.
maafisa wa Polisi wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya MAADILI katika chuo cha Polisi Zanzibar.
washiriki wa mafunzo ya MAADILI kwa maafisa wa Polisi mjini Zanzibar katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kufungua mafunzo hayo.