Sunday, November 02, 2014

Profesa Mwandosya ahitimisha ziara yake ya siku sita nchini Ethiopia kwa kukagua ujenzi wa Ofisi za Bonde la Mto Abay - White Nile



Profesa Mwandosya ahitimisha ziara yake ya siku sita nchini Ethiopia kwa kukagua ujenzi wa Ofisi za Bonde la Mto Abay - White Nile
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya leo amemaliza ziara yake ya siku sita nchini Ethiopia kwa kukagua ujenzi wa Ofisi za Bonde la Mto Abay (White Nile),kutembelea chanzo cha Mto Abay,na kutembelea maporomoko maarufu ya Mto Abay (White Nile).
Waziri Mwandosya,kushoto,akiwa na Mhaidrolijia Mengistu,Mkurugenzi Mkuu wa Bone la Mto Abay baada ya kukagua kazi zinazoendelea za ujenzi wa Makao Makuu ya Bonde mjini Bahar Dar, Amhara.
Waziri Mwandosya kwenye mti uliopandwa na mwakilishi wa Tanzania wakati wa kuweka jiwe la msingi wa Jengo wakati wa sherehe za Siku ya Nile, mwaka 2013.
Waziri Mwandosya,kushoto,na Mhaidrolojia Mengistu, kulia,na Mama Lucy Mwandosya,katikati,wakiwa kwenye maporomoko ya Mto Abay,yaliyo 'Kebele'ya Tis Abay.
Waziri Mwandosya na Mama Lucy Mwandosya wakiwa na wenyeji wao wa Gish Abay, Wilaya ya Sekela,chanzo cha Mto Blue Nile, kilicho kilomita 150 kutoka Bahar Dar.