Benki ya NMB juzi ilifungua tawi jipya maeneo ya Tandika- Dar es Salaam tawi linalokadiriwa kuhudumia Zaidi ya wateja 300 kwa siku. Tawi la NMB Tandika lipo maeneo ya Sokoni karibu na kituo cha polisi Tandika katika makutano ya mtaa wa Chihota na Ugweno.Tawi hili linatoa huduma kwa wakazi wa Tandika, Yombo,Buza,Mtongani na maeneo mengineyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Tandika. Kutoka kushoto ni; Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke Bw.Bakari Kombo , Meneja wa NMB tawi la Temeke Bw.Harold Lambileki na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salam Bw, Salie Mlay wakishuhudia uzinduzi huo.
Meneja wa tawi la NMB Tandika Bw.Cosmas Peja akimwonyesha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema idara mbali mbali zilizopo ndani ya tawi la NMB Tandika.Sambamba na uzinduzi wa tawi la NMB Tandika, NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali katika hospitali ya Wilaya ya Temeke vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5 na Madawati kwaajili ya Shule ya Sekondari Tandika yenye thamani ya Shilingi Milioni 5.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akiongea na Fatuma Said Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Tandika mara baada ya kupokea madawati kutoka NMB wakati mwanafunzi Joachim Richard akisikiliza kwa makini.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akipokea sehemu ya vifaa vya Hospitali kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salam Bw, Salie Mlay wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali ya Temeke iliyofanyika leo katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es salam.Kwanza kushoto ni: ni; Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke Bw.Bakari Kombo na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dk.Amaan Malima wakishuhudia makabidhiano.