Thursday, November 13, 2014

NHIF YAJENGA KITUO KIKUBWA CHA KISASA CHA UTAFITI WA MAGONJWA NA TIBA UDOM MKOANI DODOMA.





NHIF YAJENGA KITUO KIKUBWA CHA KISASA CHA UTAFITI WA MAGONJWA NA TIBA UDOM MKOANI DODOMA.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na ujenzi wa mradi mkubwa wa hospitali ya kisasa iliyopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.

Kwa mujibu wa Profesa Shaban Mlacha,amesema kuwa kituo hicho kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi /Utafiti na Tiba, yakiwemo ya figo,akaongeza kusema kuwa kina maabara ya kisasa na vifaa vya kisasa huku kukiwa na vyumba 40 vya madaktari.

Profesa Mlacha amesema kuwa ,kuwapo kwa hospitali hiyo itakayojengwa, itachangia si tu katika kufanya utafiti wa magonjwa na kutibia lakini pia itatoa nafasi kwa wanafunzi wa kitivo cha tiba UDOM na walimu wao kufanya mazoezi yanayostahili na kuonesha ubingwa wao.  

Baadhi ya Wahariri wa Habari kutoka nyombo mbalimbali hapa nchini,wakitoka nje ya Jengo la hospitali ya kisasa iliopo ndani ya chuo cha UDOM kama lionekanavyo pichani,ambalo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho kukamilika,Kaimu Mkuu wa Chuo  hicho  cha  Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha,amesema kuwa hospitali hiyo inatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mnamo januari 2015  mwakani .Mradi huo umegharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36 zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya UDOM,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa hospitali ya kisasa iliyopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Pichani ni Mshaurii wa mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya UDOM,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo ya kisasa iliyopo ndani ya chuo hicho cha UDOM,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa ujenzi wake umegharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.