Wednesday, November 19, 2014

MHE.SPIKA ANNE MAKINDA ASHIRIKI MKUTANO WA IPU UMOJA WA MATAIFA


MHE.SPIKA ANNE MAKINDA ASHIRIKI MKUTANO WA IPU UMOJA WA MATAIFA
Na Mwandishi Maalum, New York 
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, jana jumatatu, imeanza mkutano wake wa pili na wa siku mbili unaofanyika hapa Umoja wa Mataifa. 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ( Mb) ni miongoni mwa washiriki wa Kamati hiyo ya Maandalizi ukiwahusisha maspika kadhaa kutoka mabunge mbalimbali duniani.
Katika mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Inter-Parliamentary Union ( IPU), wajumbe wa kamati hiyo wanajadili mapendekezo ya Maudhui na Tamko la Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika mwaka 2015. 
Aidha wajumbe hao wanatarajiwa pia katika siku mbili hizi kutoa uamuzi wapi kutakakofanyikia mkutano huo. 
Maudhui na Tamko la mkutano huo wa Nne pamoja na mambo mengine yanatarajiwa kuwa yatazingatia vipaumbele au mambo muhimu na ya msingi ya mahitajo ya mwanadamu katika dunia ya sasa. 
 Mambo ambayo pia ni ajenda muhimu katika Umoja wa Mataifa Baadhi ya mambo hayo na ambayo wajumbe wa kamati ya Maandalizi wanayapitia ni pamoja na, tathimini ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs), Mapokeo ya Agenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015, na maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa wa Umoja wa Mataifa. 
Katika siku ya kwanza ya mkutano wao wajumbe wamesikiliza thathmini ya utekelezaji wa MDGs, tathmini iliyotolewa na Spika wa Bunge la Iceland ambaye ameainisha mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa malengo hayo ambayo yanafikia ukingoni mwakani. 
Pamoja na kusikiliza tathimini ya MDGs, Maspika hao pia wamepata fursa ya kubadilishana mawazo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja anayehusika na SDGs, 
 Bi Amina Mohammed ambaye ametoa muhtasari wa ajenda na malengo mapya ya SDGs baada ya 2015. Katika maelezo yake Bi Amina ametilia mkazo ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali na nafasi ya Mabunge katika utekelezaji wa SDGs huku akisisitiza kwamba changamoto kubwa na muhimu katika utekelezaji wa SDGs hizo ni suala na uwezeshaji wa raslimali fedha, suala ambalo amesema linahitaji ushirikiano wa pamoja katika kulipatia muelekeo wake. 
Aidha amewaeleza wajumbe wa Kamati kuwa Maspika na wabunge katika kila Bunge duniani kote wanapashwa kuwa weledi na wenye ufahamu mkubwa kuhusu SDGs yenye ajenda 17 na malengo 169 kwa kuwa wao ndio wawakilishi halisi wa wananchi waliowachagua. 
 Akasisitiza kuwa wabunge wanapashwa kushirikiana kikamilifu na serikali katika utekelezaji wa SDGs na huku au kubemba ujumbe wa mambo muhimu na ya msingi kwa mahitajimasuala ambayo ni muhimu kwa maisha yana Maspika kadhaa ambao ni wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabungo utaofanyika mwakani.
 Mhe. Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ( Mb) akifuatilia majadiliano yaMkutano wa  Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, Mkutano  huu wa siku mbili unafanyika hapa Umoja wa Mataifa.
 Mhe. Spika akibadilisha mawazo na   viongozi wa IPU
  Mhe. Spika akisalimiana na  Spika wa Bunge la India
Mhe, Spika  Anne Makinda akisalimia kwa furaha na  Spika wa Bunge la Uruguay