Monday, November 10, 2014

MASHINDANO YA MASHUA YA MERCEDES BENZ CUP 2014 YAFANA JIJINI DAR




MASHINDANO YA MASHUA YA MERCEDES BENZ CUP 2014 YAFANA JIJINI DAR
mashua
Moja ya mashua ikisukumwa kurejeshwa katika eneo lake la hifadhi baada ya kumaliza mashindano hayo.

Na Mwandishi wetu
MICHUANO ya siku 2 mwaka ya waendesha mashua za kisasa kuwania kombe la Mercedes Benz kwa mwaka huu imemalizika juzi jioni kwa waendesha mashua Al Bush akisaidia na Pugwash wakitwaa ushindi wa jumla na kutwaa kombe la Mercedes Benz.

Waendesha mashua hao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba 2653 wakikabidhiwa kombe hilo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO, Wayne McIntosh ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.

Akizungumzia mashindano hayo Mratibu wa waendesha mashua hao Michael Sulzar alisema yalikuwa na ushindani mkubwa na kwamba ingawa siku ya kwanza bahari ilikuwa shwari siku ya pili bahari ilikuwa chafu na kufanya wenye mashua kuwa na kazi ya ziada.
Alisema kwa kawaida mchezo huo unakuwa mtamu pale ambapo bahari inakuwa 'ngumu' ambapo waendesha mashua hao ni kama vile wanataka kutemwa kutoka kwenye mashua, hivyo wakilazimika kutumia maarifa yao kuidhibiti.
mratibu
Mratibu wa waendesha mashua Michael Sulzar akitangaza matokeo ya mashindano ya kuwania kombe la Mercedes Benz 2014 yaliyofanyika katikati ya wiki. Jumla ya timu kumi na nne (Mashua) zilishiriki katika michuano hiyo ya siku mbili.

Pamoja na washindi hao wa jumla ambao walikuwa katika mashua ya kisasa zaidi yenye Tanga mithili ya baluni washindi wengine ni Tony Hughes na Richard Stanley wakiendesha mashua Popo bawa yenye namba 2648 aina ya Hobie Tiger.


Mshindi wa tatu alikuwa Cyrille Girardin akiwa na Olivier Praz waliokuwa na mashua ya Theluji namba 72 aina ya Hobie 16.

Michael Sulzer na Andreas Schimidt wao walipata tuzo ya wawili waliofanya vyema. Wawili hao walikuwa katika mashua Die Wilde 13 yenye namba 1659 aina ya Nacra Infusion.
Aliyetwaa tuzo ya uanamichezo bora ni Mark Henderson na Shane Rumbold waliokuwa katika mashua Shark aina ya Hobie tiger.
kombe
Waendesha mashua Al Bush na mwenzake Pugwash wakiwa na kombe la ushindi la Mashindano ya mashua ya siku mbili ya kombe la Mercedes Benz yaliyofanyika jijini Dar es salaam Yatch Club.Washindi hao walikuwa wakiendesha mashua yao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba 2653.Walikabidhiwa kombe hilo hivi karibuni na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh (kulia) ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.Wa Pili kulia ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.

Mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida alikuwa David Scott akiwa na Christina waliokuwa na mahsua Alphacrucis yenye namba112483 aina ya Hobie16. Mshindi wa pili wenye mashua Polo aina ya Hobie 16 yenye namba 111206 Andrew Boyd na Kim Troll.
Mshindi wa tatu alikuwa Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren waliokuwa katika mashua namba 2657 aina ya Hobie Tiger iliyojulikana kama 1.

Jumla ya Mashua 14 zilishindana katika michezo iliyoandaliwa katika klabu ya Yatch ya Dare s salaam Msasani.

Baada ya shamrashamra za kupeana vikombe na tuzo nyingine Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh alipata nafasi ya kuzungumzia michuano hiyo ambayo imekuwa ikidhaminiwa na Mercedes Benz kwa miaka zaidi ya sita sasa.
mtoto
Mtoto wa mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida David Scott (ambaye aliendesha mashua hiyo akiwa na Christina) akimsalimia Ofisa Mtendaji mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh kabla ya kukabidhiwa tuzo ya wazazi wake ya ushindi.
tuzo
Mark Henderson na Shane Rumbold wakikabidhiwa tuzo ya uanamichezo bora, walikuwa katika Mashua Shark aina ya Hobie Tiger.
ofisa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh akizungumza kabla ya kukabidhi kombe la Mercedes Benz kwa washindi wa jumla Al Bush na mwenzake Pugwash. Michuano hiyo ilianzia na kumalizikia Dar Yatch Club Msasani. Kulia aliyebeba kombe hilo ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.