MAKATIBU wa Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Moshi Vijijini wametishia kubwaga manyanga na kurudisha kadi zao ikiwa Katibu wao wa Wilaya ataendelea na jitihada za kutaka kukigawa chama kwa kumuandaa mtu wake kwa ajili ya kugombea Ubunge mwaka 2015.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao ngazi ya kata katika wilaya ya Moshi vijijini, walisema migogoro na malumbano ndani ya CCM imekuwa chanzo cha wapinzani kushinda kiurahisi katika Jimbo la Vunjo. Mmoja wa viongozi wa Makatibu hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema, lazima wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka na siyo viongozi kuwachagulia mgombea.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao ngazi ya kata katika wilaya ya Moshi vijijini, walisema migogoro na malumbano ndani ya CCM imekuwa chanzo cha wapinzani kushinda kiurahisi katika Jimbo la Vunjo. Mmoja wa viongozi wa Makatibu hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema, lazima wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka na siyo viongozi kuwachagulia mgombea.
Wakizungumza mjini humo,makada hao ambao walikataa kutajwa majina yao kwa sababu za kuepusha malumbano, walidai kuwa muda mrefu Katibu wao wa Wilaya amekuwa akifanya jitahada za kuhakikisha mtu wake anayemtaka anapita mwaka 2015.
Mmoja wa viongozi hao ngazi ya kata, alisema Katibu wao wa Wilaya amekuwa hawasikilizi, huku akitumiwa na watu wenye fedha kuwapigia debe wagombea wao wanaowataka hususani katika kuwania ubunge mwakani.
"Tumekuwa tukimshauri huyu Katibu wetu, lakini hatusikilizi na kuna mtu ambaye mwaka 2010, alikiyumbisha chama na sasa amerudi tena akiwa na mgombea wake na hali ikiendelea hivi chama kitashindwa tena mwakani'', alisema mmoja wa Makatibu Kata
Alisema kuna kada ambaye anaandaliwa ingawa kwa sasa yupo nje ya wilaya hiyo ili aje kugombea ubunge na kwamba mpango huo unaratibiwa na watu wenye fedha.
Aliongeza kuwa wafanyabiashara wasiokitakia mema CCM wanataka wasimamishe mtu ambaye hakubaliki kwa lengo la kukiangusha ili wapinzani waweze kushindwa kiulaini..
Mmoja wa mwanachana wa CCM, katika jimbo la Vunjo alisema, umefika wakati viuongozi kukaa pembeni na kwaachia wanachama wenyewe waamue kumpitisha mgombea wanayemtaka. Alisema CCM ni chama ambacho kinajali uhuru wa kila mtu, na umefika wakati vijana kupewa kipaumbele katika nafasi za uwakilishi ukiwamo ubunge hapo mwakani.
Katibu wa CCM katika wilaya ya Moshi Vijijini, Miriam Kaaya akizungumzia tuhuma hizo, alikanusha madai ya viongozi hao wa Kata na kusema kwamba malalamiko yote yanajadiliwa ndani ya vikao. Alisema hana mgogoro wowote na makada wenzake wa CCM na kwamba siku zote amekuwa akitaka kila mtu anayestahili haki aipate bila mizengwe.
Alisema hana mpango wa kumbeba mgombea yoyote kwa kuwa muda wa kutafuta wagombea haujafika na kwamba hivi sasa wanashughulika na chaguzi za serikali za mitaa.