Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Dawa za Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin Yuan akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan.
Ujumbe wa Zanzibar Ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif ukifanya mazungumzo na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi katika Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.
Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uongozi wa Manispaa ya Mji wa Haikou ukiongozwa na Meya wa Mji Huo Mstahiki NI Qiang.
Mwenyekiti wa Kiwanda cha kusindika bidhaa za nazi pamoja na matunda kiliopo Haikuu Bwana Huang Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao la nazi. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Kulia yake ni Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na Waziri wa Habari Mh. Sai Ali Mbarouk. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.