Monday, November 24, 2014

Katibu Mkuu wa UVCCM apata mapokezi ya Kihistoria Mbinga


Katibu Mkuu wa UVCCM apata mapokezi ya Kihistoria Mbinga

10253914_742044062537178_1342623994266714427_n

Katibu mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndugu Sixtus Mapunda amepata makubwa wilayani Mbinga yaliyoacha gumzo kubwa wilayani hapo. Mapunda ambaye alitoke wilaya ya Nyasa amepokelewa kwa kishindo kikubwa na viongozi wa CCM pamoja na mamia ya wananchi wa wilaya ya Mbinga ambako ndipo alikozaliwa.

Mapunda ameingia Mbinga jana akitokea wilaya ya Nyasa ambapo ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano (5) Mkoani Ruvuma. Ziara ambayo inalenga kukagua na kuhamasisha ujenzi na uimara wa jumuiya mkoani humo pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi ya mwaka 2010-2015.

Katika hotuba yake Katibu Mkuu amewataka wananchi wa Mbinga kujitokeza kwa wingi na kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotegemewa kufanyika mapema mwezi ujao pamoja na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.

10444427_742046809203570_7347108009995380053_n

Pia Katibu Mkuu, Mapunda amemtembelea Mzee Constantine O. Millinga mmoja wa waasisi kumi na watano (15) walioanzisha Chama Cha Ukombozi cha TANU wakiongozwa na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mnamo tarehe 7.7 1954. Mzee Millinga ni miongoni mwa wawili kati ya waasisi hao ambao wako hai mpaka hivi sasa.

Mapunda ametoa wito kwaWatanzania, wananchama wa Chama Cha Mapinduzi na hasa Vijana wa Taifa hili, kuwaenzi na kuwatembelea wazee ambao ni waasisi, wazalendo wa kweli na wapigania uhuru wa nchi hii, ambao wametuwekea misingi ya Umoja na Utaifa ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya amani na utulivu.

Katibu Mkuu huyo wa UVCCM anaendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambapo atatembelea wilaya ya Namtumbo na baadae Songea Mjini ambako atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika wilaya hiyo ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.

10616255_742006742540910_7821578982643513671_n

mapunda

10408715_742006699207581_2836796389115477846_n