Wednesday, November 26, 2014

Kamishna wa Madini afungua mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake.


Kamishna wa Madini afungua mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake.
Na Teresia Mhagama 
Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Paul Masanja amefungua rasmi mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake 15 wa kitanzania waliopata ufadhili wa masomo hayo ambayo ni matunda ya harambee iliyoanzishwa na Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha mwaka 2012. 
Mafunzo hayo ya ukataji madini yatakayowawezesha wanafunzi husika kukata madini na kuyachonga katika maumbile ya kuvutia yatakuwa yakitolewa kwa muda wa miezi Sita katika Kituo cha Jimolojia (TGC) kilichopo jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
 Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini yanayoendeshwa katika Kituo cha Jimolojia (TGC) jijini Arusha, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesela (wa nne kutoka kulia), Meneja wa Uthaminishaji Madini kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), George Kaseza (wa pili kutoka kulia) na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (wa kwanza kulia).
 Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (wa nne kutoka kushoto mstari wa pili) akiwa katika picha ya pamoja  na Wanafunzi 15 waliopata ufadhili  wa masomo ya uongezaji thamani madini yanayoendeshwa katika Kituo cha Jimolojia (TGC) jijini Arusha. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera (wa pili kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA),  Sammy Mollel (wa tatu kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito Arusha, (AGF), Peter Pereirra(wa tatu kulia mstari wa pili) Mwalimu anayefundisha masomo hayo kutoka nchini Sri Lanka, Pathmasiri  Alwis (wa kwanza kushoto mstari wa pili) pamoja na watendaji Kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kituo cha Jimolojia (TGC) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).
 Baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini wakionesha baadhi ya madini ya vito ambayo yamekatwa na kuchongwa katika maumbo ya kuvutia baada ya kupata elimu hiyo kutoka kwa mwalimu Pathmasiri Alwis wa nchini Sri Lanka. Pamoja nao ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja ( wa pili kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesela (wa kwanza kushoto),Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA),  Sammy Mollel (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito Arusha, (AGF), Peter Pereirra(wa kwanza kulia mstari wa pili)
 Kamishna Msaidizi wa  Madini, Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane  akiangalia jinsi  wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini  wakichonga madini ya vito katika maumbo ya kuvutia katika Kituo cha Jimolojia (TGC) Arusha kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini  akijifunza kuchonga madini ya vito ili yawe katika umbo la kuvutia kabla ya kumfikia mtumiaji.