.Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela akikagua vifaa vya maabara pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Tukuyu, Tiberi Sambala HALMASHAURI ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imejipanga kuhakikisha inatekeleza agizo la Rais la ujenzi wa Maabara katika Shule za Sekondari ifikapo Novemba 15 Mwaka huu linakuwa limekamilika. Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela, alipokuwa akipokea msaada wa mifuko ya Saruji kutoka kampuni ya uzalishaji na uchimbaji wa gesi Mkaa ya TOL Gases limited na Mradi wa huduma ya umeme vijijini (REA) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara wilayani hapo. Meela alisema msaada huo umefika katika kipindi muafaka ambapo Halmashauri inajipanga kuhakikisha agizo la ais la kujenga maabaraNchi nzima linakamilika hadi ifikapo Novemba 15 mwaka huu ambapo alisema tayari ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia 80. Akiyashukuru makampuni hayo Meela alisema ni makampuni yanayoshughulika na masomo ya sayansi hivyo michango yao ni kuongeza chachu ya upatikanaji wa wataalamu katika shughuli zao wanazozifanya ili waweze kuongeza wengine wengi kupitia shule za Kata. Alisema katika kutekeleza agizo hilo, Wakuu wa Idara wote wamepelekwa kwenye maeneo ya ujenzi ili kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha malengo yanatimia kama ilivyopangwa ambapo Halmashauri ina sule 43 ambazo zinatakiwa kujengwa maabara. Aliongeza kuwa baadhi ya watu wanafikiri agizo la Raisi ni ujenzi wa majengo ya maabara pekee lakini Halmashauri yake imeshakamilisha ujenzi wa majengo na kilichobaki ni miundombinu inayopaswa kuwekwa kwenye maabara ili ianze kufanya kazi jambo ambalo alisema litakuwa limekamilisha kabla ya muda. Alisema hivi sasa wanajipanga kuhakikisha wanajaza vifaa vya maabara ikiwa ni pamoja na kununua mitungi ya Gesi upatikanaji wa umeme kwa shule zilizopitiwa na Grid ya Taifa huku wakiomba msaada Wizarani wa kupata Umeme wa Jua kwa shule zilizoko vijijini ili maabara ziweze kufanya kazi kisasa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya State Grid Company ltd inayohusika na mradi wa umeme wa Rea, Andrew Mwaipaja, alisema wameguswa kuchangia kutokana na kinachohimizwa kunahusiana na kazi yao ya kuitaji mafundi na wataalamu wa sayansi ambao watapatikana baada ya kuwa na maabara nzuri. Alisema Kampuni yake imeguswa na kuamua kuchangia mifuko 100 ya Saruji pamoja na Seiling Bod 80 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni tatu ambavyo vilikabidiwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe. Naye Mkurugenzi wa Fedha wa TOL Gases ltd, Evarist Tilafu, alisema wamuamua kuchangia mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya shilingi Milioni 1.7 kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii ambayo ipo jirani na eneo wanalifanyia kazi. Mwisho. Na Mbeya yetu |