Monday, October 13, 2014

Waziri Mkuu Pinda mgeni rasmi mechi ya viongozi wa dini jijini Dar

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa timu ya Mshikamano,ambapo timu hiyo imenyukwa goli moja dhidi ya timu ya Amani,mchezo huo wenye lengo la kuimarisha na kudumuisha amani na mshikamano tulionao umefanyika katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali
Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa timu ya Amani,ambayo imeibuka kinara katika mashindano hayo kwa kuichapa timu ya Mshikamano goli moja.Mchezo huo wenye lengo la kuimarisha na kudumisha amani na mshikamano tulionao umefanyika katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar  ukijumuisha viongozi mbalimbali wa dini ya Kikristo na Kiislamu,ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa dini na serikali walihudhuria.
 Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Amani
 Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Mshikamano
 Sehemu ya umati wa watu waliokuwepo kushuhudia mechi ya Amani na Mshikamano,iliyofayika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa.
 Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akizungumza jambo mbele ya wachezaji wa timu ya Amani na Mshikamano,zilizoundwa mahsusi katika kuadhimisha siku ya amani duniani,ambapo  viongozi wa dini uliojumuisha Masheikh, Maimamu, Maaskofu, Wachungaji na Mapadre.Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,Shoto kwake ni Mkuu wa  Mkoa wa Jiji la Dar,Mh.Said Meck Sadick na Rais wa TFF,Bwana Jamal Malinzi.

Katika mchezo huo wa kujenga amani na mshikamano uliopo nchini,Mwamuzi msaidizi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Mh. Said Meck Sadick na mwamuzi aliyeshika kipyenga alikuwa ni Kamishna wa Kanda Maalumu, Seleman Kova 
Mkuu wa Mkoa wa jiji la  Dar, Mh.Said Meck Sadick  ambaye alizungumza machache na kumkaribisha Mgeni Rasmi wa mchezo huo wa Viongozi wa Dini kati ya Amani na Mshikamano,Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda pichani kulia. 
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo,akizungumza machache. 
 Rais wa TFF,Bwan, Jamal Malinzi akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar, Mh.Said Meck Sadick  ambaye alizungumza macheche na kumkaribisha Mgeni Rasmi wa mchezo huo wa Viongozi wa Dini kati ya Amani na Mshikamano,Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda.