Balozi Tuvako Manoni ( nyuma) akiwa katika picha pamoja na wanafunzi wenye umri kati ya miaka 11-14 kutoka shule za Montessori waliofika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara ya Mafunzo yao yanayolenga kuwajengea uwezo wa kujielimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea katika Umoja wa Mataifa. Katika ziara hiyo pamoja na kutembelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa pia hutembelea baadhi ya Wakilishi za kudumu kwa lengo la kutaka kufahamu vipaumbele vya nchi hizo na ushiriki wao katika mijadala mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na pia hupenda kujifunza historia ya nchi hiyo. katika picha wapo pia walimu walioambatana nao katika ziara hiyo. Anaoneka pia Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu . Bw. Noel Kaganda anayeratibu shughuli za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na ambaye alipewa jukumu la kuwaeleza wanafunzi hao na walimu wao vipaumbele vya Tanzania katika Umoja wa Mataifa pamoja na kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi.