Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari (kushoto) akiangalia wananchi wake wakiendelea na uchimbaji wa mtaro wa kupitisha Mabomba ya Maji ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kuhakikisha Ahadi ya maji kwa wananchi wa Manyata na Nganana kata ya Usa River inatimia.
Mbunge Nassari aliingia kazini kuanzia asubuhi mpaka jioni. Mradi huu umetoa maji umbali wa kilomita 9 toka kwenye chanzo (Uraki). Wananchi wa Arumeru walikuwa wanakunywa maji ya majaruba ya mpunga kwa miaka yote kabla ya mradi huo ulioasisiwa na Mbinge wa Jimbo hilo,Mh. Joshua Nassari
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mhe. Joshua Nassari akishiriki kazi za mikono za kuchimba mtaro wa maji, kutandaza mabomba na kuzindua mradi wa maji aliouanzisha katika vitongoji Vya Manyata na Nganana.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mhe. Joshua Nassari akichota maji katika moja ya bombo mara baada ya kuzindua mradi wa maji aliouanzisha jimboni hapo.
Furaha ya kupata maji ilikuwa ni ya kila mwanakijiji katika eneo hilo.