Viongozi wa timu za Simba na Yanga, Geofrey Nyange Kaburu, kushoto ambaye ni Makamu wa Rais Simba na Mohamed Bhinda, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga (kulia) wakivuta kamba kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 inayoendeshwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Uzinduzi huo rasmi kwa wadau wa Simba na Yanga ulifanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja wa bia hiyo, George Kavishe na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Bi Kushilla Thomas (aliyevaa suruali nyeupe).
Mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakivuta kamba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 ya Kilimanjaro Premium Lager kwa wadau wa Simba na Yanga uliofanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo chini ya Kilimanjaro Premium Lager .
Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga wakicheza muziki wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 kwa wadau wa timu hizo mbili katika hafla iliyofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga wakiingiakwenye viwanja vya Leaders wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 kwa wadau wa timu hizo mbili katika hafla iliyofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa timu za Simba na Yanga, Geofrey Nyange Kaburu, kushoto ambaye ni Makamu wa Rais Simba na Mohamed Bhinda, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga (kulia) wakishindana kupiga danadana kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 inayoendeshwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Uzinduzi huo ni kwaajili ya wadau wa timu hizo ulifanyika jana viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo.