Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi waliofika kwa wingi kwenye ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada wakifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9 ,ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mbunge wa Kawe,Mhe Halima Mdee mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada (wa pili kulia),Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe (kulia) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana. |
Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS,Injinia Patrick Mfugale akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Yasunori Onish akizungumza machache kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada akitoa hotuba yake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada kwa kutoa hotuba yake nzuni na kwa lugha ya Kiswahili wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki akizungumza na kutia msisitizo wa kuwatana watu wanaoharibu miundombinu ya barabara kuacha mara moja,kwa kufanya hivyo ni uhalifu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe.
"Siasa sio Ugomvi" hapa ni wanachana wa vyama viwili tofauti vya siasa wakijumuika pamoja katika kuyarudi magoma.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa tayari tayari kumrekodi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo.