Wednesday, October 08, 2014

TASAF YAPIGA HODI KANDA YA ZIWA VICTORIA.





TASAF YAPIGA HODI KANDA YA ZIWA VICTORIA.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza  hatua ya kutambua kaya maskini katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Tanga, Morogoro,Pwani na Simiyu ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN unaoratibiwa na mfuko huo nchini kote kwa awamu. Akifungua warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa wilaya ya Maswa ,Mkuu wa wilaya hiyo Luteni Mstaafu Abdallah Kihato ametoa wito kwa wananchi kuzingatia miongozo ya TASAF ili waweze kunufaika na mpango huo. 

Amesema serikali wilayani humo itatoa ushirikiano kwa wataalamu wa TASAF na watendaji wengine ili zoezi la kuzibaini kaya maskini liweze kufanikiwa. Kwa upande wake meneja fedha wa TASAF Bw. Njego Nyamukowa kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa mafanikio makubwa .
 Mtaalam kutoka TASAF Bw. Hamis Kikweppe akitoa maelezo juu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa timu ya wawezeshajio wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. (2)
 Meneja wa Fedha wa TASAF Bw.Njego Nyamuko aliyeshika kipaza sauti mbele akitoa maelezo juu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoendeshwa na TASAF katika warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa wilaya ya Maswa.

 Mkuu  wa wilaya ya Maswa Luteni Mstaafu Abdallah Kihato akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya mpango wa kunusuru kaya maskini katika wilaya ya Maswa.