Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujengewa uelewa wa mpango wa kunusureu kaya maskini unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.
Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF,Bw. Alphonce Kyariga (aliyesimama) akifungua warsha ya kuwajengea uelewa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga maafisa ufuatiliaji TA wa mamlaka za utekelezaji PAAs kwa pya kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujengewa uelewa wa mpango wa kunusureu kaya maskini unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujengewa uelewa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiowa na TASAF wakiwa katika ukumbi wa TEC mjini DSM kupata maelezo ya mpango huo kabla ya kwenye katika maeneo ya utekelezaji katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Mwanza, Shinyanga Na Simiyu.
Mmoja wa wawezeshaji wa warsha ya kujen gewa uelewa maafisa ufuatiliaji wapya wa mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN Bi.Woisso kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM .
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaanza awamu ya nne (wave 4) ya zoezi la kubaini kaya maskini katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Morogoro, Tanga na Pwani Oktoba 6 Mwaka huu.
Katika maandalizi hayo TASAF imeanza warsha kwa ajili ya wawezeshaji wa Kitaifa, wataalamu wa ufuatiliaji TAs na watumishi wa makao makuu (TMU) ambao watakwenda kufanya kazi kwenye maeneo ya utekelezaji wa Mradi katika mikoa hiyo.
Akifungua warsha hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi wa uratibu wa TASAF Bw. Alphonce Kyariga amesema kazi ya utambuzi wa kaya maskini ni nyeti na inayotakiwa kufanywa kwa umakini mkubwa ili kupunguza uwezekano wa kutozibaini kaya za walengwa.
Amessistiza kuwa miongozo na taratibu zilizowekwa na TASAF zinapaswa kufuatwa ili hatimaye zoezi hilo liwe la mafanikio makubwa kama inavyotarajiwa.