Friday, October 03, 2014

Amref kuandaa hafla ya chakula cha jioni kuchangia mafunzo ya wakunga nchini Tanzania



Amref kuandaa hafla ya chakula cha jioni kuchangia mafunzo ya wakunga nchini Tanzania
Meneja Mradi Uboreshaji wa Uzazi Salama wa Chama cha Wakunga Tanzania (Tama), Martha Rimoy, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, wakati Taasisi ya Amref Health Africa, ilipokuwa ikielezea kuhusu kuandaa hafla ya chakula cha jioni, Oktoba 9 kwenye Hoteli ya Serena, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufundishia wakunga ili kuokoa afya ya  mama na mtoto, katika kampeni ijulikanayo kama 'Stand up for African Mother'. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkazi wa taasisi hiyo, Dk. Festus Iloko, Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benk M, wafadhili wa kampeni hiyo, Jacquelin Woiso na Naibu Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Rita Noronha.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Africa nchini, Dk. Festus Iloko, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusu hafla ya chakula cha jioni, itakayofanyika Oktoba 9 kwenye Hoteli ya Serena, ili kuchangisha fedha za kufundishia wakunga kwa ajili afya ya  mama na mtoto, katika kampeni ijulikanayo kama 'Stand up for African Mother'. Kulia ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benk M, mmoja wa wafadhili wa kampeni hiyo, Jacquelin Woiso.
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benk M, mmoja wa wafadhili wa kampeni hiyo, Jacquelin Woiso, akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Amref Health Africa, wakiwa kwenye mkutano huo.
Naibu Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Rita Noronha, akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo.Picha na Kassim Mbarouk.