Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
Baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo kabla ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini Arusha.
Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi
Na Asteria Muhozya, Arusha.
Tanzania imeeleza mipango yake ya kuendeleza masuala yanayohusu nishati jadidifu mbele ya Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimtaifa la Jotoardhi linaloendelea jijjini Arusha.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho kwa niaba ya Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Jotoardhi Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Paul Kiwele amesema kuwa lengo la kukutana kwa kamati hiyo ni kuzungumzia hatua zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao.
Bw. Kiwele ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo ameeleza kuwa, lengo jingine la kikao hicho ni kuangalia faida zilizopatikana kupitia nishati hiyo pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na kuona namna bora ya kuzitatua.
Ameongeza kuwa, pendekezo la nchi wanachama kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza masuala ya jotoardhi katika nchi zao ikiwemo ya kifedha limepitishwa na mashirika kadhaa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhifadhi wa Mazingira ( UNEP) na Umoja wa nchi zilizo katika bonde la Ufa (ARGEO).
Aidha, Bw, Kiwele ameongeza kuwa, kikao hicho kimeamua kuipa nafasi Tanzania kusaidiwa kuendeleza masuala ya jotoardhi katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la Ngozi, Mkoani Mbeya.
Kikao hicho cha Kamati ya Watoa Maamuzi ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea katika kongamano la tano la jotoardhi ambapo linakwenda sambamba na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusu masuala ya jotoardhi ikiwemo masuala ya utafiti, uchorongaji na masuala ya fedha.
Kongamano hilo litafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal jijini Arusha na litawashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali duniani.