Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana akisalimiana na Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Dkt. James Diu.
Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Uchumi(TCAA) Dkt. James Diu , akitoa hotuba kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa AATO Bi Margreth Kyarwenda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) , kinachomilikiwa na TCAA wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Baadhi ya wataalamu wa sekta ya Usafiri wa Anga toka nchi ya Senegal wakifuatilia kwa karibu mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Baadhi ya wataalamu wa sekta ya Usafiri wa Anga Tanzania wakifuatilia kwa karibu mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana. J. Mbwana (katikati) akiwasikilza wajumbe wa mkutano wa AATO , baada ya kufungua mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Wengine kutoka kushoto ni mjumbe wa Bodi TCAA, Yussuf . M. Ali, Mkurugenzi Idara Udhibiti Uchumi , TCAA, Dkt. James Diu , Rais wa AATO Tchagbele Sadamba na Mjumbe wa Bodi TCAA. Hanif. M. Malik
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shabaan Mwinjaka(Kushoto) akifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa AATO Bi Margreth Kyarwenda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) , kinachomilikiwa na TCAA wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika, Mbwana J. Mbwana (watano kutoka Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
-----
Oktoba 1-3.
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) utakaofanyika Zanzibar.
Mkutano huo wa siku tatu, kuanzia Oktoba 1-3, utakutanisha vyuo vya mafunzo ya usafiri wa anga, wataalamu wa sekta na taasisi nyingine zinazohusiana na masuala ya usafiri wa anga. Kauli mbiu ya Mkutano ni "Uhuishwaji na Viwango vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga kwa Usalama wa Usafiri wa Anga Barani Afrika na Kwingineko".
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe atafungua mkutano huo wakati, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano , Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt Juma Duni Haji atakuwa mgeni rasmi wakati wa kufungwa kwa mkutano.
Wakati wa mkutano huo wajumbe watajadiliana kuhusu ushirikiano wa vyuo vya usafiri wa anga, hatua zilizofikiwa katika kuanzisha vituo vya mfano(center of excellence) vya mafunzo ya usafiri wa anga na uhaba wa wataalam wa usafiri wa anga barani Afrika, changamoto zinazotokana na taaluma mpya za usafiri wa anga na mstakabali wa AATO.
Wajumbe hao pia watapata fursa ya kutembelea maeneo ya utalii huko Zanzibar. Maeneo hayo ni pamoja na mashamba ya viungo, kisiwa cha Prison maarufu kwa kobe wakubwa na eneo la mji mkongwe wa Zanzibar.
AATO ilizinduliwa mwaka 2013 huko Abuja, Nigeria kufuatia mapendekezo ya mkutano maalumu wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO AFI- RAN) mwaka 2008 nchini Afrika Kusini. Mapendekezo yalizitaka taasisi za mafunzo ya usafiri wa anga kuwa na mikutano ya pamoja kwa lengo la kuboresha ushirikiano, viwango, ubora na kuhuisha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Malengo mkakati ya AATO ni pamoja na kuwa na sauti ya pamoja ya vyuo wanachama na kuhimiza vyuo hivyo kuendeshwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.
Vyuo wanachama wa AATO vinapata manufaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye ushirikiano na vyuo wanachama, fursa ya kujitangaza na kutambulika zaidi, kuwa na mitaala inayokidhi viwango. Faida nyingine ni kupata taarifa sahihi kuhusu sekta ya usafiri wa anga
Chuo cha usafiri wa Anga Tanzania(CATC) ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa AATO pia ni mwanachama wa baraza la AATO ikiwakilisha nchi za Afrika Mashariki. AATO ina vyuo wanachama 30.
Margareth Kyarwenda
KNY
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA(TCAA).