Thursday, October 16, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI



images
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LUSEKERO AMBILIKILE (36), TINGO NA MKAZI WA BULYAGA – TUKUYU ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.920 BSW AINA YA FUSO TIPPER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE SETH HAMAD KUPINDUKA ENEO LA KATUMBA WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:40 JIONI HUKO MAENEO YA KATUMBA, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.

DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA – RUNGWE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 03 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JORIN WILLIAD [JINSI YA KIKE] MKAZI WA GHANA JIJINI MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE NDOO YA MAJI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA 09:45 ASUBUHI HUKO MAENEO YA GHANA MASHARIKI, KATA YA GHANA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA KIFO HICHO NI BAADA YA MTOTO HUYO KUTAKA KUTOA KIATU CHAKE KILICHOKUWA NDANI YA NDOO NA KATIKA HARAKA HIZO NDIPO ALITUMBUKIA KWENYE NDOO HIYO ILIYOKUWA NA MAJI NA KUFARIKI DUNIA.
MWILI WA NAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA, KUFUKIA MASHIMO KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA IYUNGA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GRACE MBUILONGO (48) AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO MAENEO YA IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.