Thursday, October 16, 2014

STATOIL YAGUNDUA KISIMA KINGINE CHA GESI ASILI


STATOIL YAGUNDUA KISIMA KINGINE CHA GESI ASILI
Kampuni ya Statoil ikishirikiana na Exxon Mobil, imetangaza kugundulika kwa gesi asilia katika eneo jipya la Giligiliani-1 katika ukanda wa Bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Statoil na kuchapishwa katika tovuti yao, ugunduzi huo katika eneo la Giligiliani-1, ni ongezeko la futi za ujazo 1.2 trilioni za gesi asilia ambazo sasa zitafanya kuwe na jumla ya futi trilioni 21 za ujazo za gesi asilia katika Kitalu Namba 2.
Katika nukuu yake juu ya utafiti huo, makamu wa rais mwandamizi wa kampuni ya Statoil, Nick Maden alisema eneo hilo lipo magharibi mwa Kitalu Namba 2 na kina cha cha urefu wa baharini cha mita 2,500.
"Ugunduzi huu ni uthibitisho kuwa eneo hilo lina hazina ya nishati ya gesi. Kwa kipimo chetu cha mafanikio, tumeona kuwa Tanzania inazidi kufungua na imekuwa na bahati kwa upande huu wa gesi asilia ambao utaleta mafanikio kwa nchi na sisi washirika kutokana na programu hii," alisema Maden.
Alisema kutokana na programu hiyo, wana matarajio makubwa ya kuendelea kupata kiasi kikubwa cha gesi nchini kadiri utafiti unavyozidi kufanyika.
Alitaja vitalu hivyo ambavyo vimegunduliwa katika eneo hilo kuwa ni Maden alisema ni pamoja na Zafarani, Lavani, Tangawizi, Mronge na Piri.
Statoil inatumia leseni ya Kitalu Namba 2 kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),inamiliki asilimia 65 na zingine 35 zinaenda serikalini.
Statoil ilianza kazi nchini tangu mwaka 2007 baada ya kushinda zabuni ya kitalu namba mbili