Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam NAIBU KATIBU MKUU TAIFA NA KATIBU MKUU WA BODI ya CHAMA CHA UJENZI WA TAIFA, NRA (NATIONAL RECONSTRUCTION ALLIANCE), Mhe HASSAN KISABYA ALMAS, ametoa pole kwa wananchi wa mkoa wa kigoma na Uongozi Mzima wa mkoa kwa msiba mzito uliowapata baada ya watu zaidi ya kumi kupoteza maisha kwa ajali ya boti.
Ndugu Kisabya alisema, ajali ni jambo lisilotarajiwa na kuwataka ndugu jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao kuna na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Ndugu kisabya,aliomba uongozi wa mkoa kufuatilia kwa ukaribu sana ajaili hiyo ili kubaini chanzo cha ajali hiyo na kuweka mikakati thabiti ili ajali kama hiyo isitokee tena.
Kwa upande wa wahudumu wa safari hizo aliwaasa kutochukua idadi kubwa wa watu tofauti na uwezo wa chombo husika ili kuepusha majanga kama hayo, Ndugu kisabya alitoa shukurani kwa askari wetu wa Jeshi la wananchi walioshirikiana na wananchi katika kuopoa maiti na Mali za wahanga wa ajali hiyo,pia alitoa shukurani kwa uongozi wa SERIKALI ya mkoa Mzima kwa kuonyesha mshikamano Mkubwa katika ajali hiyo.
Katika salamu zake ,ndugu kisabya alisema, "NIMEGUSWA SANA NA MKASA HUU, NI AJALI MBAYA KUTOKEA ,NAUNGANA NA WAFIWA, WANANCHI WOTE,NA UONGOZI WA MKOA WA KIGOMA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU,HASA UKIZINGATIA NI NYUMBANI KWETU,PIA WALIOPOTEZA MAISHA NI WATANZANIA WAJENZI WA TAIFA NA NI HAZINA YA NGUVU KAZI YA TAIFA"
Mungu awalaze pema marehemu wote,MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI KIGOMA!