Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya Safari Wezeshwa msimu wa nne uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji wa programu hiyo, Joseph Migunda.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akiwaonyesha kipeperushi kinachoonyesha kitika cha shilingi 2200,000 000/= zitakazogawiwa kwa wajasiliamali wakati wa uzinduzi wa programu ya Safari Wezeshwa msimu wa nne uliozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imeziduwa rasmi programu yake ya Safari Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo Nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alifafanuwa ya kwamba " programu hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini kwani itarahisisha kazi kwa kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi".
Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.
Bw. Oscar alifafanuwa kuwa, Programu hii itafanyika takribani mikoa yote Nchini ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia leo kupitia mtandao wa www.wezeshwa.co.tz na baadae kusambazwa katika mabohari na viwanda vya TBL nchi nzima.
Hii itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi Nae Jaji kutoka TABDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa "Zoezi hili linahusisha majaji wenye utaalamu na wenye umakini kwa namna moja au nyingine.
Hivyo aliomba wajasiriamali wote wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii".