Thursday, October 23, 2014

PSPF YAANDAA CHAKULA CHA JIONI KWA WALIMU MJINI MOROGORO



PSPF YAANDAA CHAKULA CHA JIONI KWA WALIMU MJINI MOROGORO
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Afande Leonard Paul, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya wachezaji wa timu ya polisi mkoani Morogoro na wajumbe wa  idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro, Alhamisi Oktoba 23, 2014.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, Jumatano Oktoba 22, 2014, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wachezaji hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo mjini Morogoro Oktoba 22, 2014. Wajumbe hao wanatarajiwa kubhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo ili kuwaelimisha walimu faida wanazoweza kupata endapo watajiunga na Mfuko huo.

 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Seme, akiwasalimia walimu ambao ni wajumbe kutoka idara ya utumishi wa walimu wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa wajumbe hao wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF, ili kuelezea shughuli mbaklimbali na faida unazoweza kupata unapojiunga na Mfuko huo. Semina hiyo ilifanyika mkoani Morogoro
Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro. Picha na Masogange