Tuesday, October 07, 2014

NSSF FURSA SEMINA YASHAMIRI SIKU YA IDD EL HAJJ MJINI DODOMA



NSSF FURSA SEMINA YASHAMIRI SIKU YA IDD EL HAJJ MJINI DODOMA
Ikiwa ni muendelezo wa Semina za Fursa zinazoendelea katika mikoa mbalimbali, licha ya kuwa ni siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj tarehe 05/10/2014, Semina ya Fursa yashamiri mjini Dodoma na kuvutia umati mkubwa wa watu.

Umati huo ulivutiwa sana na huduma na mafao yatolewayo na NSSF kama vile Matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake na mikopo kupitia Saccos.

NSSF iliwasihi watu wajiunge na mfuko huu ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao.

Semina ya Fursa Dodoma ilirushwa Live na kituo cha Redio cha Clouds FM katika mkoa wa Dodoma  na hivyo kuwapa Fursa hata wale walioshindwa kufika ukumbini kusikia mada zilizotolewa popote walipo ndani ya mkoa wa Dodoma.

Semina hii ilihudhuriwa na wajasiriamali, wanafunzi wa vyuo vikuu na wakulima wa mkoa wa Dodoma wapatao 900.

Semina hizi za NSSF Fursa chini ya usimamizi wa Clouds Media zimefanyika katka mikoa ya Geita, Songea, Morogoro, Mbeya, Singida na Dodoma. 


Semina hizi zonaendelea ili kuwapa FURSA Watanzania wa mikoa mingine 6 ya Mtwara, Mwanza, Kagera, Arusha, Moshi na Dar es Salam kujiandikisha na NSSF na kujipatia mafao mbalimbali.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa kwanza kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma,  Kirondera Nyabuyenze (wa pili kulia) na Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba  (wa tatu kulia) wakiwa katika semina ya Fursa Dodoma.
 Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (wa tatu kushoto) na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kushoto) wakifutilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa katika semina ya Fursa Dodoma.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa Dodoma. 
 Baadhi ya watu waliohudhulia semina hiyo wakiskiliza kwa makini Fursa zitolewazo na NSSF.
Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa watu waliohudhuria semina hiyo.
 Mwanamuziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi akiwahamasisha wananchi waliohudhuria semina hiyo wajiunge na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae. Kushoto ni Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba. 
 Maofisa wa NSSF, Gabriel Nkakatisi (kushoto) na Anna Nguzo wakiandikisha wanachama wapya baada ya kumalizika kwa semina ya Fursa iliyofanyika siku ya sikukuu ya Idd El Hajj mjini Dodoma.
Baadhi ya watu wakijiandikisha katika banda la NSSF baada ya semina ya Fursa Dodoma.