Tuesday, October 28, 2014

NAIBU WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA MAFUNZO YALIYOANDALIWA NA RITA NA NBS.



NAIBU WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA MAFUNZO YALIYOANDALIWA NA RITA NA NBS.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki Jana alifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Serikali watakaoshiriki Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu zake Nchini.

Mhe. Kairuki amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia maelekezo ya Wakufunzi kwa makini ili waweze kuandaa mpango kazi utakaotekelezeka ili kuleta mabadiliko makubwa katika Hali ya kiwango cha Usajili wa Matukio Muhimu kwa mwanadamu (Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka) hivyo kuchochea maendeleo nchini.

Mafunzo Hayo ya Siku Tano yanafanyika katika Hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo na yanahusisha Wakurugenzi na Maofisa waandamizi kutoka Idara za Sera na Mipango wa Wizara ambazo ni Wadau wakuu wa Usajili wa wananchi, Maofisa wa RITA, NBS na idara nyingine za Serikali.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mr. Yacob Zewodi, Bi Celia De Klerk na Bi. Thandi Makale ambao ni Washauri Waelekezi wa Kimataifa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki akifungua Mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Serikali watakaoshiriki Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu zake Nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Phillip Saliboko akitoa maelezo kuhusu Mafunzo yali yofunguliwa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki katika picha ya pamoja na Washiriki.
Mafunzo yanaendelea...