Thursday, October 23, 2014

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE NA MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA YA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE NCHINI CHINA


MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE NA MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA YA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE NCHINI CHINA
2Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi tarehe 21.10.2014.3Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe 22.10.2014. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo.4Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.5Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la  CNOOC la China katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.6Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.78Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014.9Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.10Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.11Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya picha Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe 22.10.2014.
unnamedMke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake kwenye kijiji cha sanaa za Afrika mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika kumbukumbu yake.
PICHA NA JOHN  LUKUWI.