Meneja Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Rajabu Kinande, akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Amina Kassim, na Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe.
Meneja Kanda ya Dar es Salaam wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Amina Kassim akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe na Kulia ni Meneja wa LAPF Kanda ya Kaskazini. Rajabu Kinande.
---
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, yamekamilika ambapo mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 700 toka nchini na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliud Sanga, amesema maadalizi yote ya mkutano huo, wenye kauli mbiu ya "Maadhimisho ya Miaka 70 ya Ukuaji na Huduma Bora, LAPF", yamekamilika ambapo ambapo utakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF.
Bwana Sanga amesema Mfuko wa LAPF ndio mfuko unaoongozwa sii tuu kwa kutoa mafao bora, bali pia ndio mfuko unaoongoza kwa kuwa na afya bora kabisa ambapo kwa sasa una rasilimali zenye thamani ya shilingi bilioni 700, LAPF ndio mfuko unaoongoza kukua kwa kasi zaidi ambapo unakuwa kwa asilimia 21 kwa mwaka!.
Ameendelea kutoa sifa za LAPF kuwa ni pamoja na kuwa ndio mfuko unaolipa kwa haraka zaidi, ambapo mstafuu kama anastaafu kesho, LAPF wao wanalipa jana!.
Bwana Sanga hakuishia hapo, amesema LAPF ndio mfuko unaoongoza kwa utunzani wa mahesabu kati ya mifuko yote kwa mujibu wa NBAA, na ndio mfuko unaokuwa kwa kasi zaidi kwa mujibu wa SSRA!.
Mkutano huo, utafunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia, na Kufungwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka.